ELIMIKA KISUKARI SI UGONJWA WA KUDUMU - MAINTAIN YOUR HEALTH

Trending

Thursday, February 7, 2019

ELIMIKA KISUKARI SI UGONJWA WA KUDUMU


ELIMIKA KISUKARI SI UGONJWA WA KUDUMU 



Duniani takwimu zinaonyesha kila sekunde 10 mtu mmoja mwenye kisukari hufariki na zaidi ya watu 40,000 wenye kisukari Tanzania hukatwa miguu pia zaidi ya watu milioni 422 wana kisukari duniani hivyo kupelekea ugonjwa huu kushika nafasi ya 5 kama kisababishi cha vifo duniani. Ugonjwa wa kisukari ni moja ya ugonjwa unaowahangaisha watu wengi duniani kwani mtu anaweza akaishi na ugonjwa huu kwa muda mrefu takribani miaka 5 na kuendelea bila hata ya kujijua kuwa anatatizo la kisukari, kwa kiwango kikubwa hutokana na mfumo wa maisha wa mtu atakavyoamua kuishi, hivyo huu ugonjwa unaweza ukampata kila mtu mtoto kwa mtu mzima

ugonjwa wa kisukari ni nini? ni ugonjwa unaotokana pale insulin inaposhidwa kubalansi  sukari, ambayo homoni ya insulin hutengenezwa kwenye kongosho(pancreas) na kongosho inaposhindwa kufanya kazi vizuri hupelekea homoni ya insulin kupungua au kuongezeka na ndo hapo hutokea utofauti wa kisukari, pia ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu. Ikumbukwe kuwa kisukari huwapata mpaka watu wasio wanene(wembamba) na mama wajawazito
                 
 VISABABISHI VINAVYOPELEKEA MTU APATE UGONJWA WA KISUKARI.
Vyanzo vinavyopelekea mtu aweze kuwa mwathirika wa ugonjwa wa kisukali endapo asipovizingatia kwa umakini vyazo vikuu vipo vya aina mbili ambazo ni mfumo wa maisha na kurithi.
Mfumo wa maisha. Hii imekuwa sababu kubwa ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa haraka zaidi kuliko chochote na hii inatokana na ulaji (vyakula na vinywaji), kutokana na uandaaji wa vyakula kutoka vinalimwa hadi kuja kuingia kinywani mwa binadamu imekuwa ni changamoto kwa sababu ya kemikali zinazotumika kutunzia vyakula lakini pia na mtu yeye mwenyewe kama anapenda kula vitu vitamu vitamu ni kirahisi zaidi mtu huyo kuathirika kwa ugonjwa huu, uchunguzi uliofanyika huko marekani unasema kuwa mtu anaependa kula vyakula vyenye sukari nyingi au vitamu kuwa anakiwango kikubwa cha bacteria wabaya mwilini na hao bacteria hupendelea kula vitu vitamu kwahiyo inakuwa ni kirahisi sana kuchochea homone na kushidwa kwa kongosho kubalansi kiwango cha sukari mwilini.
·         Unene (obesity). Uzito uliopitiza kiwago ni moja ya sababu zinazopelekea mtu kuugua ugonjwa wa kisukari kwa sababu mwili wa mtu mnene unakuwa na sukari nyingi au kuwa na glucose nyingi
·         Kazi za ofisini. Mtu anaefanya kazi za kukaa kwa muda mrefu bila kufanya mazoezi anakuwa na hatari ya kuwa na kiwango kingi cha sukari kwa sababu anakuwa hafanyi zoezi lolote la kuweza kuunguza mafuta na sukari mwilini mwake hii ni tofauti na miaka ya 1980’s miaka hiyo watu wengi shughuri zao zilikuwa siyo za ofisini knazi zao nyingi zilikuwa za kuushughurisha mwili na hivyo ilikuwa ni kirahisi zaidi kuunguza mafuta bila hata ya kufanya mazoezi hii ni tofauti na sasa.
Kurithi. Haijafahamika kuwa nini sababu inayopelekea kurithi huu lakini kama kwenye ukoo kulikuwa na mgonjwa wa kisukari hivyo ugonjwa usishangae mtu kuugua kisukari bila hata ya hizo visababishi vya juu.
Baada ya kujifunza juu ya visababishi vinavyopelekea kuadhirika kwa ugonjwa wa kisukari hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mtu anapokuwa na kisukari anakuwa na dalili zipi, zifuatazo ni dalili za mtu alie na ugonjwa wa kisukari.




DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI.
Unapoona hizi dalili siyo kwamba ni moja kwa moja tayari una ugonjwa wa kisukari ni vema zaidi ukafika hospital ukachukua vipimo pale unapoona baadhi ya dalili ili kupata uhakika wa afya ya mwili wako japo dalili za mtu mwenye kisukali ni kama zifuatazo;
i.              Kukojoa mara kwa mara. Mtu mwenye kisukari hukojoa mara kwa mara ni pamoja na insulin kushidwa kubalansi sukari mwilini na kufanya sukari iwepo kwenye damu nyingi ndo maana huchochea kukojoa mara kwa mara.
ii.            Kiu isiyoisha. hii ni kwa sababu mwili wako unapoteza maji mengi kwa njia ya mkojo na hivyo husababisha mwili uhitaji mengi isivyo kawaida.
iii.           Njaa kali. Ni kwasababu insulin yako haiwezi kubeba glucose mwilini mwako au hauna insulin ya kutosha ambayo husaidia kubeba lishe zilizomo kwa vyakula na kukufanya upate vitamin vya kutosha.
iv.           Kuongezeka uzito. Hii inatokana na dalili ya kusikia njaa kali na hivyo humfanya mtu kula vyakula vingi na kwenda kuchochea homoni mwilini kufanya kazi pasivyo kawaida na ndio hapo unamkuta mgonjwa wa kisukali ananenepa tu.
v.            Kupungua uzito. Hupungua uzito hasa pale mgonjwa wa kisukari anapokosa hamu ya kula na hivyo mwili wake hukosa lishe au virutubisha na kupoteza madini mengi mwilini mwake na seli zake hukosa chanzo cha chakula.
vi.           Kukojoa mkojo na wadudu kama sisimizi na nzi kuuzingira. Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa bacteria wabaya wanapenda vitu vitamu hivyo na wadudu nao hivyo hivyo mgonjwa wa kisukari huwa anatoa mkojo wenye sukari nyingi na ndio maana huo mkojo unakuwa rafiki na wadudu.
vii.          Kuchoka. Ili mtu awe na nguvu za kutosha ni lazima sukari ibadirishwe kutoka kwenye vyakula kwenda kwenye misuri, hivyo basi mgonjwa wa kisukari, sukari yake hubaki kwenye damu na siyo kwenye misuli na ndo maana huchoka bila hata kufanya kazi yoyote anaweza kuamka asubuhi kutoka kitandani na anakuwa kachoka.

MADHARA KWA MGONJWA WA KISUKARI NA BAADHI YA VIUNGO VINAVYOATHIRIKA ZAIDI.
Kupenda vitu vitamu hususani jamii ya sukari huwa ni tamu sana kwenye ulimi lakini changamoto inakuja kule inakoelekea kwa ajili ya kutunzwa na kutumika, hapo ndo husababisha changamoto mbalimbali mwilini hasa kwenye baadhi ya viungo vya mwili. Yafuatayo ni madhara ya sukari inapozidi mwili na kiwango sahihi cha sukari inayotakiwa mwili pale unapokuwa umekula chakula:
·         vidonda vya miguuni (diabetes foots). Ugonjwa wa kisukari huathiri miguuni hasa pale unapopata ganzi inapelekea kushidwa kuhisi maumivu hivyo hata ukipata jeraha au mchubuko unakuwa huhisi maumivu ya aina yoyote unakuwa hauna tofauti na aliechomwa sindano ya ganzi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji,
vidonda vya mtu mwenye kisukari ni vigumu sana kupona kwa sababu damu inakuwa haifiki ya kutoshakwenye kidonda na asilimia kubwa bacteria wabaya
huanza kukishambulia kwa kasi kwa sababu kinakuwa ni kitamu 
 
kwa bacteria na kinaonekana kuwa na malengelenge ya mafuta na hao bacteria hushambulia kwa kasi hivyo kusababisha kuongezeka kwa kidonda na mwishoe kukatwa endapo hatawahi huduma mapema ya kujikinga.
·         Kutokuona vizuri au mtoto wa jicho. Mishipa ya kwenye macho huwa ni midogo midogo sana na iko laini sana ukiliganisha na mishipa ya sehemu zingine za mwili hivyo inapoingiliwa na sukari damu hushidwa kupita ya kutosha sehemu za macho na kumfanya mtu awe anaona ukungu ukungu au kutokuona kabisa.
·         Madhara ya figo. Figo inapokuwa imezidiwa na kiwago kingi cha sukari hulazimika kupunguza maji ya ziada na utengenezaji wa calcium kwa ajili ya kulinda mifupa hivyo sukari nyingi kukimbilia kwenye damu na baadaye huwa sumu mwilini.
·         Kiharusi (stroke). Kwa kuwa madhara ya sukari mojawapo ni kudhoofisha mishipa kwenye mwili hivyo mtu wa kisukari ana hatari kubwa ya kupata stroke kwa sababu baadhi ya mishipa kwenye ubongo huathiriwa na kukosa uwezo wa kupitisha damu ya kutosha na mwishoe kupasuka na kusababisha kiharusi.
·         Maradhi ya moyo. Vyanzo vya mishipa huanzia kwenye moyo na kusambaa pande zingine za mwili, moyo huathiriwa na ugonjwa wa kisukari kwa sababu sukari hudhoofisha mishipa na kumfanya mtu kuwa dhaifu hivyo kama damu haipiti ya kutosha kwenye mishipa inakuwa ni kirahisi kupata magonjwa ya moyo kama vile moyo kupanuka, moyo kuwa na tundo pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.
·         Kwa wanaume kuishiwa nguvu za kiume. Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume kwa sababu mfumo wa uzazi wa mwanaume umeundwa kwa mishipa na misuli, kama patakuwa hakupati ujazo mzuri wa damu inakuwa ni rahisi sana kushidwa kushiriki tendo ndoa na wengi wao wanapopatwa na hali kama hii huigiwa na presha au msongo wa mawazo na kuibuia matatizo mengine tena.
 Hayo ni baadhi ya madhara anayopatwa mtu mwenye kisukari japo anaweza kupatwa na changamoto zingine nyingi kwenye mwili wake na kumpelekea kupata shida awe mtoto au mtu mzima, lakini jinsi kwa kukosa uelewa na umakini zaidi kundi la watu wengi huishia kukatwa baadhi ya viungo na mwishoe kifo.
Lakini ujue kuwa kama ugonjwa siyo wa kuambukizwa itashidikanaje kuuzuia ili usiendelee kukudhuru usipatwe na madhara makubwa ya kiafya , moja ya suluhisho ambalo limesaidia watu kadha wa kadha linalotokana na mimea, mitishamba mboga mboga ambazo husaidia kurudisha ubora wa mwili kama mwanzo na badae unakuwa na afya njema jifunze kuhusu hii program inavyofanya kazi.

PROGRAM YA KURUDISHA KIWANGO SAWA CHA SUKARI MWILINI NA KUIMARISHA AFYA YA MWILI.



Changamoto ya kisukari inaweza kabisa kuepukika endapo tu ukiwa na nia ya kujiimarisha bila kukata tamaa ya kuitumia hii program, kama wengine imeweza kuwaimarisha na wakawa vizuri kwanini isiwe kwako pia. Kuna ubora gani kwa hii program.

  • Inasaidia kuogeza uwezo wa kinga mwilini na kukupa nguvu hivyo kuondoa uchovu wa bila sababu 


  • Inaimarisha uwezo wa tendo la ndoa kwa pande zote kwa wanaume na kwa wanawake, pia inaimarisha tezi dume kwa wanaume.
  • Inaondowa hatari ya kupata kiharusi kwani hewa(oxygen) na damu vitakuwa inapita vyema kwenye ubongo

    •  Inasaidia kuondoa sumu mwilini na kubalansi kiwango cha sukari mwilini kama imepanda zaidi huishusha na kama imeshuka zaidi huipandisha.
    •  Inasaidia kuondoa bacteria wabaya na kuwapandisha uwezo wa utendaji kazi wa bacteria wazuri.
    • Inasaidia kuhakikisha mzunguko wa damu uko sawa na ujazo ulio sawa kwenye mishipa
    • Endapo kama tayari mwathirika anavidonda sehemu yoyote ya mwili hufanya kazi kukausha vidonda na kuondoa bila kuonyesha makovu.
    •  Inaisaidia kongosho utoaji wa insulin kufanya kazi vizuri
    •  Inamchanganyiko wa mbogamboga ambazo hufanya kazi ya kukupa damu na nyuzi nyuzi ili kusaidia upataji wa choo usiwe wa shida.
    • Inasaidia kuondoa matatizo ya macho na kuondoa mtoto wa jicho bila kukwanguliwa kwa kutumia vifaa
    Hakuna changamoto ya kudumu chini ya jua vyote vina suluhisho, amuwa kuwa wa tofauti kwa kutafuta suluhisho kwa matendo. Wasiliana nasi ili kujua zaidi kuhusu kisukari na suluhisho lake kwani hatukuumbwa ili tuteseke na kisukari bali tuishi wenye afya tele.

     +255738 651373   /    +255657 461124   &   janemlay762@gmail.com



    5 comments:

    1. during morning its raising up to 13,but afternoon comes to 9, and i tried to control only by diet....Morning cup of milk,two eggs or sometimes bread baking almond flour/pumpkin flour....lunch meat/fish with vegetables till full and dinner a glass of milk with avocardo..so is it okey and how can i drop it during morning..

      ReplyDelete
    2. Thanks for well information about diabetes to prevent

      ReplyDelete
    3. Kiwango cha sukari inatakiwa ngapi.

      ReplyDelete
    4. Kiwango cha sukari inatakiwa ngapi.

      ReplyDelete
    5. Kiwango cha sukari inatakiwa ngapi.

      ReplyDelete

    Post Top Ad

    Responsive Ads Here